WANANCHI KAHAMA WAIONYOOSHEA KIDOLE TANESCO KUKATIKAKATIKA KWA UMEME.Baadhi ya wananchi wilayani Kahama wamelalamikia shirika la Umeme TANESCO wilayani humo kwa kukata UMEME kwenye baadhi ya maeneo bila taarifa, jambo ambalo limekuwa likisababisha usumbufu kwa wananchi.

Wakizungumza na Kijukuu Blog leo baadhi ya wananchi hao  wamesema mara nyingi maeneo yao yamekuwa na adha ya kukatika kwa umeme huku maeneo mengine yakipata huduma hiyo.

Akijibu tuhuma hizo Meneja wa TANESCO wilaya ya Kahama KING FOKANYA amesema hali hiyo inatokana na matengenezo ya mitambo yanayoendelea kwa baadhi ya maeneo kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika. 

Hata hivyo FOKANYA amekanusha taarifa za baadhi ya watu wanaosema kuwa TRASFORMA za zamani zinasababisha kukatika  kwa umeme, na kusema kuwa sio kweli bali ni marekebisho yanayofanyika kwenye maeneo mbalimbali.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata