WAKULIMA WILAYANI KAHAMA WATAKIWA KUACHA KULIMA KWA MAZOEA.

Wakulima wilayani Kahama wameshauriwa kuachana na kilimo cha mazoea badala yake watumie mbegu bora za kisasa pamoja na kupanda kwa kutumia utaalam ili wapate mazao ya kutosha.

Akizungumza katika ukaguzi wa mashamba ya mfano ya mahindi na pamba katika Kata ya Mapamba, Halmashauri ya Ushetu mapema wiki hii, Afisa Kilimo wa Kata hiyo, MATHEW JOHN amesema ni vyema mkulima akaachana na kilimo cha mazoea ili kukuza kilimo cha jembe la mkono.

Mkuu wa wilaya ya Kahama, FADHILI NKURLU ambaye pamoja na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mapamba, EVELIN ERASTO wanamiliki mashamba hayo ya Mfano, amesema ameandaa shamba hilo ili  kutoa hamasa kwa wakulima na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili kwa wakati.

NKURLU amewapongeza maafisa ugani wa Kata ya Mapamba kwa jitihada wazazozifanya kuhakikisha kilimo kinasonga mbele na kuwataka wakulima kuwatumia maafisa ugani kuleta mapinduzi ya kilimo chini ya kauli mbiu ya wilaya isemayo “TUKUTANE SHAMBANI”.

Kata ya Mapamba ina jumla ya wakulima 11,320, ambapo kati yao 704 wamesajiliwa kwa kilimo cha pamba Msimu huu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata