VIJANA KAHAMA WATAKIWA KUFAHAMU SHERIA YA MITANDAO YA KIJAMII.
Na Sebastin Mnakaya
KAHAMA 

Vijana wilayani Kahama mkoani Shinyanga wanatakiwa kufahamu sheria ya mitandao ya kijamii  kabla hawajaanza kuitumia ili kuepuka athari zitokanazo na kuvunja sheria hiyo. 

Hayo yamesemwa jana  mjini Kahama na  afisa mradi wa kuboresha  utawala bora katika jamii kupitia  teknolojia ya kidigitali  kutoka shirika la CABUIPA, DANIEL  MADULU wakati akifunga mafunzo ya mradi huo kwa  WARAGHABISHI kutoka wilaya ya Mbogwe.

Amesema idadi kubwa ya  vijana  hawafahamu sheria ya mtandao, na  mara nyingi wanajikuta wakivunja sheria hiyo pasipo kufahamu na hivyo kupewa  adhabu.

Baadhi wa waraghabishi waliopata mafunzo hayo wameyashukuru mashirika  yaliyowapa elimu ya sheria ya mitandao  na kuahidi kutumia mitandao hiyo kwa lengo la kuimarisha uchumi wao.

Mradi huo unatekelezwa kwa mwaka mmoja katika wilaya ya MBOGWE   na unatekelezwa na Mashirika  ya CABUIPA na OXFAM, ambapo unalenga kuielimisha jamii kufahamu taarifa kupitia mitandao ya kijamii ili kuinua uchumi wao.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata