SINGAPORE: MABASI BILA DEREVA KUANZA KUFANYA KAZI 2022

Mabasi bila dereva yanatarajia kuanza kufanya kazi mwaka 2022 nchini Singapore.

Waziri wa miundombinu Khaw Boon Wan wakati wa ufunguzi wa jaribio la basi la kwanza lisilokuwa na dereva nchini humo,ametangaza kuwa kuanzia 2022 mabasi hayo yataingia barabarani.

Ripoti zinaonyesha kuwa huenda miaka mitano ijayo wakazi wa miji tofauti nchini humo wakapendelea zaidi kutumia mabasi yasiyokuwa na dereva hasa kuendea makazini.

Teknolojia hiyo itatumika sana katika miji yenye idadi kubwa ya watu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata