RC SHINYANGA AINGIA VIJIJINI KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF ILIYOBORESHWA.

 WANANCHI Mkoani Shinyanga wametakiwa kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii  CHF iliyoboreshwa ili waweza kupata matibabu ya uhakika kwa muda wa mwaka mmoja tangu kujiunga na mfuko huo.

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Terack wakati akiongea na wananchi wa kata ya Kilago katika mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Shule ya msingi Kilago.

Terack amesema ugonjwa haubishi hodi hivyo ukiwa na kadi ya Mfuko wa Afya ya jamii CHF unaweza kupata matibabu wakati wote na kuongeza kuwa kwa wasiyo na pesa wanaweza kuuza kuku mmoja tu na kupata pesa itakoyowawezesha kujiunga na mfuko huo.

Sambamba na hayo Telack amesema kuwa Gharama ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya jamii ni  Shilingi elfu kumi inamrahisishia mwananchi kupata huduma ya matibabu kwa mwaka mzima na kumwondelea usumbufu wa kutoa pesa nyingi kwa wakati mmoja ili kupatiwa huduma.

Kwa upande wake meneja wa Mradi wa tuimarishe Afya (HPSS) mkoa Shinyanga Dr Harun Kasale amesema kuwa CHF iliyoboreshwa inampa nafasi mteja kupata matibabu katika vituo  vyote vya afya vya mkoa tofauti na ilivyokuwa  CHF ya zamani.

Kwa mujibu wa Taarifa ya kata ya Kilago iliyosomwa mbele ya mkuu wa mkoa na Afisa elimu kata bwana Benard Masala zaidi ya kaya Elfu moja mia tano zimejiunga katika mfuko wa CHF sawa na watu elfu mbili mia nne themanini na moja.

Kata ya Kilago yenye vijiji sita ina jumla ya kaya elfu mbili mia tatu themanini na saba na idadi ya watu watu wapatao elfu kumi na nne miasaba thelathini na nane.

MATUKIO KATIKA PICHA:

 KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KAHAMA TIMOTH NDANYA AKIMKARIBISHA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BI ZAINAB TELACK MWENYE KIREMBA CHA NJANO KUZUNGUMZA NA WANANCHI WA KATA YA KILAGO.
 BAADHI YA WAKUU WA IDARA PAMOJA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA  NA MKOA WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO.

MEZA KUU WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO ULIOFANYIKA KATIKA SHULE YA MSINGI KILAGO.


 WAKUU WA IDARA PAMOJA NA KAMATI YAULINZI NA USALAMA WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO.

 AFISA ELIMU KATA YA KILAGO BWANA BERNARD MASALA AKISOMA RISALA MBELE YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA KUHUSU MIPANGO YA MAENDELEO YA KATA.

 MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BI ZAINAB TELACK MWENYE KIREMBA CHA NJANO AKIW NA KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ROBERT NKWELA MWENYE MIWANI WAKIKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KINACHOJENGWA KATIKA KIJIJI CHA NYANEMBE.
MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AKITOA MAAGIZO KWA VIONGOZI WA KIJIJI CHA NYANEMBE NA OFISI YA MKURUGENZI KUHAKIKISHA WANAPIMA ENEO LA KITUO CHA AFYA ILI KUONDOA MIGOGORO YA ARDHI KATI YA WANAKIJIJI NA SERIKALI.
 HILI NI ENEO LA JENGO LA UPASUAJI LINALOJENGWA KATIKA KIJIJI CHA NANYEMBE.
 UJENZI WA JENGO  LA OPD UKINDELEA KATIKA KIJIJI CHA NYANEMBE AMBAPO MKANDARASI AMEHAIDI KULIKABIDHI MWISHONI MWA MWEZI WA KUMI NA MBILI.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata