NSSF YATOA SEMINA KWA UMOJA WA WAANDISHI WA HABARI KAHAMA,KUACHA KAZI KWA WAFANYAKAZI KWATAJWA KUWA NI CHANGAMOTO.

Tatizo la kuacha kazi kwa wafanyakazi katika taasisi mbalimbali zilizojiunga na Mifuko ya hifadhi ya jamii ni changamoto inayowafanya wanachama washindwe kuendelea kubaki kwenye mifuko hiyo na hivyo kujitoa na kudai mafao kabla ya kufikia umri wa kustaafu.

Hayo yamesemwa jana na  afisa mwandamizi wa uendeshaji wa shirika la hifadhi ya jamii NSSF tawi la Kahama, ERNEST RUSATO wakati wa semina kwa umoja wa waandishi wa habari wilayani Kahama KJF kilichofanyika mjini Kahama.

Amesema hali hiyo inatokana na wanancha hao kukosa ajira baada ya kuacha kazi ama kufukuzwa na waajiri wao hivyo kuamua kujiajiri wao wenyewe kwa kutumia  mafao ambayo waliweka kwenye mifuko hiyo.

Naye Meneja wa NSSF wilaya ya  Kahama, MZEE MUSHI amewataka waandishi wa habari wilayani Kahama, hasa waliopo kwenye umoja wa KJF, kuendelea kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuwa na  maisha bora wakati wa uzee.

Amesema Tasinia ya Habari ni kitengo ambacho kinawafikia wananchi kwa wakati hivyo ni vyema kutengeneza vipandi pamoja na kuandika habari zenye kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kuweka akiba kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii.

Mwenyekiti wa Umoja wa Waandishi wa Habari Kahama  WILLIAM BUNDALA(KIJUKUU)  akizungumza kwa niaba ya wenzake, amewapongeza NSSF  kuwa karibu na jamii na kwamba amewashauri kutumia vyombo vya habari ili kuyafikia makundi mbalimbali  ya wananchi ikiwamo ya wachimbaji madini na waendesha pikipiki za abiria(Bodaboda).

Umoja wa wandishi wa  habari Kahama KJF umeanzishwa mwaka huu kwa lengo la kuimarisha umoja  na  ushirikiano miongoni mwa wanahabari na jamii   hivyo kuleta maendeleo ya haraka  katika jamii wilayani humo na taifa kwa ujumla.

 MATUKIO KATIKA PICHA:


 AFISA MWANDAMIZI WA UENDESHAJI WA SHIRIKA LA HIFADHI YA JAMII NSSF TAWI LA KAHAMA, ERNEST RUSATO AKITOA MAFUNZO KWA UMOJA WA WAANDISHI WA HABARI KAHAMA.

 WAANDISHI WA HABARI WA KAHAMA JOURNALIST FORUM WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WAKISIKILIZA KWA MAKINI HUDUMA ZITOLEWAZO NA NSSF.

 MWAKILISHI WA RADIOKWIZERA WILAYANI KAHAMA BWANA RUZIRO AKIULIZA SWALI KATIKA SEMINA HIYO.

 AFISA MWANDAMIZI WA UENDESHAJI WA SHIRIKA LA HIFADHI YA JAMII NSSF TAWI LA KAHAMA, ERNEST RUSATO AKITOA MAFUNZO KWA UMOJA WA WAANDISHI WA HABARI KAHAMA.
 WAANDISHI WA HABARI WA KAHAMA JOURNALIST FORUM WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WAKISIKILIZA KWA MAKINI HUDUMA ZITOLEWAZO NA NSSF.

 WAANDISHI WAKIENDELEA KUPATA ELIMU KUHUSU MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII NSSF.

SEMINA IKINDELEA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA SHIRIKA LA NSSF.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata