MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE AKUTWA AMEKUFA KWENYE BWAWA LA MAJI WILAYANI KAHAMA


Na Ndalike Sonda,

KAHAMA

Mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Majengo mjini Kahama ERICK SAMWEL (10) amekutwa amefiki dunia katika bwawa la Lyanzungu lilipo mtaa wa Mhongolo mjini humo.


Baadhi ya mashuhuda wamesema mwanafunzi huyo amekutwa akielea kwenye bwawa hilo ambapo juhudi za kuutoa mwili wake zilifanywa na wananchi pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mataa.


Kwa mujibu wa baba mazazi wa ERIC, SAMWEL MWANDA, mwanae alipotea tangu jana ambapo licha ya kufanya juhudi za kumtafua lakini hawakufanikiwa kumpata hadi leo walipomkuta katika bwawa hilo.


MWANDA amesema badaye walipata taarifa kuwa kuna mtoto amekutwa katika bwawa hilo na ndipo walikwenda na kuukuta mwili huo ukiwa umeopolea na wananachi.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Mhongolo EMANUEL amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kwamba tayari wamekwisha utaarifu uongozi wa juu likiwemo jeshi la Polisi, na amewataka wazazi na walezi kuwa makini kwa watoto wao.


Baadhi ya wananchi waliozungumza na Kahama fm wameiomba serikali kuweka uzio na ulinzi katika bwawa hilo ili kudhibiti vifo vya watoto vinavyotokana na kuzama wakiwa wanaogelea kwenye bwawa hilo.


Jeshi la Polisi wilayani Kahama limefika eneo la tukio na kuruhusu shughuli za mazishi kufanyika.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata