MWANAFUNZI WA CHUO CHA UHAZIRI TABORA AJINYONGA KWA KUTUMIA TAI.Mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora kinachojulikana kama UHAZILI, RAPHAEL KADESHA (22)  amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tai.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora GRAIFTON MUSHI, tukio hilo limetokea jana majira ya saa 4 asubuhi, na kwamba marehemu alitekeleza azma yake hiyo kwa kufunga tai juu ya kitanda chake na kujining’iniza.

MUSHI amesema RAPHAEL alikuwa akisoma kozi ngazi ya  Cheti cha Awali cha Utawala katika Chuo hicho.

Mkurugenzi wa Chuo hicho Dkt. RAMADHAN MARIJANI ametoa wito kwa wanachuo kuwa watulivu wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa sababu za mwanachuo huyo kujinyonga.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata