MWANAFUNZI ALIYEOKOTA BOMU LILILOUA WANAFUNZI KAGERA AJULIKANA...ALIBEBA KWENYE BEGI LA MADAFTARI

Mwanafunzi aliyeokota bomu la kutupa kwa mkono akidhani ni chuma chakavu kwa lengo la kwenda kuuza imebainika kuwa ni miongoni mwa watano waliokufa baada ya kulipuka na kujeruhi wengine 43, akiwemo mwalimu wao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Ollomi amemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Juliana Tarasisi (13).

Amesema hayo leo Alhamisi Novemba 9,2017 kuwa, mwanafunzi huyo alilitunza bomu hilo kwenye begi lake la madaftari ili kwenda kuliuza kwa mnunuzi wa chuma chakavu wakati wa mapumziko.

Wanafunzi wengine waliopoteza maisha katika tukio hilo lililotokea jana, Jumatano Novemba 8,2017 ni Evart Theonas (12) Edson Bigilimana (12), Miburo Gabriel (12), na Tumsifu Ruvugo (8).

Wanafunzi 42 wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kihinga na mwalimu wao wa darasa, Policalipo Clemency aliyekuwa darasani wakati wa tukio wamelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Rulenge.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata