MKAZI WA MAJENGO KAHAMA AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KWA KOSA LA KUUWA KWA KUKUSUDIA.Mkazi wa Majengo Wilayani Kahama JUMA ABDALA (43) leo amehukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama kuu ya Tanzanzania,Kanda ya Shinyanga kwa kosa la kumuua STEVEN BALOZI kwa  kukusudia.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, VICTORIA MAKANI baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na Mashahidi 9 wa Upande wa Jamhuri pasipo kuacha shaka yeyote.

Amesema Mahakama imemtia hatiani JUMA, Katika shauri hilo namba 14/2015 kwa kuua kwa kukusudia kwa mujibu wa kifungu namba 196 sura 16 ya kanuni ya adhabu marejeo ya mwaka 2002 ili iwe fundisho kwa Watu wengine kwenye jamii.

Kwa upande wake Wakili wa Serikali MARIGARET NDOWEKA amesema JUMA alitenda kosa hilo mwaka 2007 kwa kumuua STEVEN kwa kumpiga risasi kichwani na kisha kuiba gari lake na kutokomea kusikojulikana.

Naye Wakili wa Utetezi, FESTO LEMA ameiomba Mahakama hiyo kumpunguzia adhabu Mteja wake kwa sababu ni kosa la kwanza na anafamilia inayomtegemea hoja ambayo imetupiliwa mbali na Mahakama.

Jaji MAKANI amesema Rufaa kwa JUMA iko wazi kama hajaridhika na Hukumu hiyo .

Makahama hiyo imemaliza leo kikao chake ambapo Mashauri 9 yamesikilizwa na kutolewa maamuzi.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata