MAMA LISHE KATA YA MAJENGO KAHAMA,WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA JENGO LA KISASA.Baadhi ya mama lishe wa kata ya majengo halmashauri ya mji wa Kahama wameipongeza halmashauri hiyo kwa kuweka mradi wa jengo maalum  la mamalishe ambalo kukamilika kwake kutawasaidia akina mama hao kukua kiuchumi.

Akizungumza na Kijukuu kwa niaba ya  mama lishe wenzake REJINA LUKAS amesema kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia mama lishe kuondokana na kero wanazukumbana nazo  kwenye maeneo yao ya sasa ikiwemo ubovu wa miundombinu na mazingira hatarishi.

REJINA ameongeza kuwa kutokana na jengo hilo kuwa la kisasa litasaidia kuongeza wateja kutokana na ubora na usafi wa mazingira, ambapo itaondoa hofu ya usalama wa chakula kama ilivyo sasa katika baadhi ya migahawa ya chakula. 

Diwani wa kata ya majengo BERNARD MAHONGO amesema mradi huo unalengo la kusaidia mama lishe waliopo ndani ya kata ya majengo pekee na hivyo kukuza uchumi wao.

MAHONGO amesema jengo hilo ambalo lina vyumba 24 litagharimu shilingi milioni 148.8 hadi kukamilika kwake, ambapo vyumba 12 ni vya sehemu ya kulia chakula, na vyumba 12 ni kwaajili ya majiko na kuhifadhi vifaa.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata