MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA KUPINGA USHINDI WA KENYATTA...SASA KUAPISHWA KUWA RAIS


Mahakama ya Juu nchini Kenya imetupilia mbali kesi zilizofunguliwa na wafuasi wa NASA za kupinga ushindi wa Urais wa Uhuru Kenyatta, kwenye uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26, 2017
Kesi hiyo ambayo ilikuwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari, iliongozwa na majaji 6 akiwemo Jaji Mkuu David Maraga, na kutoa uamuzi kuwa Uhuru Kenyatta ni mshindi halali wa uchaguzi wa Oktoba 26.
Kufuatia uamuzi huo wa mahakama ya Juu nchini Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo, na kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa muhula wa pili.
Ikumbukwe uchaguzi wa marudio ulifanyika baada ya Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya Urais ya uchaguzi wa kwanza wa Agosti 8, 2017 na kutaka urudiwe mara ya pili.
Tume ya Uchaguzi imefurahia uamuzi wa Mahakama ya Juu na kusema ni dhihirisho la kujitolea kwa tume hiyo kufanikisha uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika.
Imesema kupitia taarifa kwamba inasubiri uamuzi wa kina ambao utaiongoza katika kutathmini uchaguzi huo ulivyokuwa pamoja na mipango yake ya kuimarisha uchaguzi na tume yenyewe.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata