LEMMA:TUKO TAYARI KUUZA FIGO TUPATE PESA ZA KUMTIBU LISSU.

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema hata kama gharama za  matibabu ya Tundu Lissu yakifika Trilioni  moja, watakuwa tayari kuuza figo zao.

Akizungumza jana  Novemba 18 katika kata ya Siuyu iliyopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Lema alisema utekelezaji wa  majukumu ya kisiasa ukiwa upinzani wakati huu ni ngumu kutokana na kuwindwa kila uchao.

Alisema  pamoja na ugumu huo hawajarudi nyuma na kisasi cha wasiopenda mabadiliko na wanaochukia kukosolewa   kimedhihirika  kwa vitendo alivyotendewa Lissu.

"Lissu yupo kitandani risasi mwili mzima, gharama za matibabu yake ni kubwa, lakini hata ikifika trilioni moja na tukawa hatuna fedha tutauza figo zetu kuendelea kugharamia matibabu yake" alisema Lema.

Alisema Lissu amekuwa alama ya haki katika taifa kutokana na kuamua kuwa upande wa haki.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata