JESHI LA POLISI KAHAMA KULA SAHANI MOJA NA BODA BODA WANAOPAKIA MISHIKAKI KWENDA MACHIMBO YA MWIME.Jeshi la polisi kitengo usalama barabarani wilayani Kahama limesema halitasita kuwachukulia hatua za kisheria ikiwamo kuwafikisha mahakamani waendesha pikipiki za abiria (Bodaboda)  ambao wanakiuka sheria kwa kubeba abiria zaidi ya mmoja.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo hicho wilayani Kahama, ROBERT SEWANDO wakati akizungumza na Kijukuu Blog, kuhusu madereva bodaboda wanaobeba abiria kwenda katika mgodi mdogo wa Mwime wilayani humo.

SEWANDO amesema watafanya oparesheni hiyo ili kuwakamata wanaokiuka sheria za usalama barabarani, hivyo kuwataka bodaboda kufuata sharia inayowazuia kubeba abiria zaidi ya mmoja na kuzingatia uvaaji wa kofia ngumu (Helment).

Nao baadhi ya waendesha bodaboda wanaosafirisha abiria kwenda katika machimbo hayo KASANGA JUMA,WILSON JOHN na ABDALAH LAZARO wamesema wanafanya hivyo kutokana na ushindani wa kibiashara ulipo baina yao na  vyombo vingine vinavyosafirisha abiria.

Ongezeko la waendesha bodaboda  na vyombo vingine vya usafiri kubeba abiria wanaokwenda katika Machimbo ya Mwime  limekuwa ni kubwa, na hivyo kusababisha uvunjifu wa sheria za usalama barabarani na ajali.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata