INASIKITISHA MWANAUME AUAWA KIKATILI NA KUNYOFOLEWA SEHEMU ZA SIRI KISA KUKUTWA NA MIPIRA YA KIUME MIFUKONI MWAKE

Mwanaume mmoja nchini Thailand ameuawa kikatili na mke wake kwa kukatwa na kisu sehemu zake za siri baada ya kukutwa na mipira ya kiume mfukoni.
Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Amnuay Wensila (62) alikutwa na kondom kwenye mifuko yake na mkewe baada ya kurejea nyumbani akitoka kazini. Ndipo alipoulizwa na kushindwa kutoa maelezo.

Taarifa kutoka gazeti la Post Today la nchini humo zimeeleza kuwa mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Nittaya Saengdeuan (22) alianza kumchoma kisu kwenye mwili wake kabla ya kumuua kwa kumkata sehemu zake za siri.

Baada ya kutekeleza mauaji hayo, Bi. Nittaya aliuchukua mwili wa marehemu na kuufunika kwenye pipa nje ya nyumba yao.

Awali, Nittaya alikataa kutoa ushirikiano na polisi akidai kuwa hajahusika na chochote kuhusu kifo cha mmewe akidai kuwa hata yeye alikuwa anamtafuta.

Hata hivyo, baada ya mahojiano marefu na kamanda wa polisi mjini Udon Thani,  Peerapong Wongsaman ambako tukio hilo lilikotokea alikubali kutekeleza mauji hayo.

Bi Nattaya kwenye mahojiano na Kamanda wa Polisi.

Nittaya kwenye maelezo yake amesema alichukua maamuzi ya kumkata uume mumewe baada ya kukuta kondomu kwenye mifuko yake kwani aliamini kuwa ameshasalitiwa.

“Tulifanya nae mahojiano kwa muda mrefu na mwanamke wa Amnuay Wensila (62) na amekiri kutekeleza mauaji ya mumewe kwa kumchoma sehemu zake za siri kutokana na wivu wa mapenzi na tayari taratibu za kumpeleka mahakamani zinafanywa.“amesema Kamanda Peerapong Wongsaman.

Nittaya atakamiliwa kwa kesi ya kuua kwa kukusudia na hii inakuwa sio mara ya kwanza kutokea nchini Thailand kwani mwaka 2015 liliripotiwa tukio kama hilo ambapo mwanamke mmoja alimuua mumewe kwa kumwagia tindikali akiwa usingizini baada ya kukuta meseji ya mahaba kuingia kwenye simu yake wakiwa wamelala.

Chanzo : Today Post & Linda Ikeji

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata