HAPA KAZI TU: DC NA MKURUGENZI MBOGWE WASHIRIKIANA NA WANANCHI KUENDELEZA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA SHENDA.

GEITA

SERIKALI wilayani Mbogwe mkoani Geita imewataka wananchi kujitokeza kushiriki katika shughuli za maendeleo zinazowahusu katika maeneo yao kwani hakuna mtu baki anayeweza kuleta maendeleo tofauti na wao wenyewe.

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Bi Martha Mkupasi wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha shenda,ujenzi ambao umeanza kujegwa kwa nguvu za wananchi.

Mkupasi amesema wanakijiji wote wa Kijiji cha Shenda wanatakiwa kujitokeza kushiriki miradi ya maendeleo hususan ujenzi wa Zahanati na kwamba watakaobaki  nyumbani ni wagonjwa,Watoto na wazee pekee yao.

Sambamba na hayo Mkupasi amesema kuwa ujenzi wa Zahanati hauna Chama wala dini na kwamba Shughuli za maendeleo hazina itikadi na  kutoa onyo kwa viongozi wa siasa kuacha kutumia Shughuli za maendeleo kujinadi katika majukwaa ya siasa.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Shenda wameushukuru uongozi mpya wa Kijiji chini ya mwenyekiti wa Kijiji Hicho Khalid Akida kwa kusimamia miradi ya maendeleo huku wakishukuru kuanza kwa Ujenzi wa Zahanati hiyo.

Katika hatua nyingine wananchi hao wamewashukuru Mkuu wa wilaya ya Mbogwe na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kujumuika nao katika uzinduzi wa ujenzi wa zahanati hiyo na kuongeza kuwa wawasaidie pale wanapohitaji msaada wa kiutaalamu.

Akizungumzia utaratibu mpya waliouanzisha halmashauri ya Mbogwe kufanya shughuli za Maendeleo kwa Kushirikisha wananchi mkurugenzi wa halmashauri hiyo Elius Kayandabila amesema kuwa inasaidia kupunguza gharama za matumizi ya fedha.

Kayandabila ameongeza kwa kuwataka wananchi wa Kijiji cha Shenda kushirikiana katika ujenzi wa zahanati hiyo kwani wote watanufaika na uwepo wa zahanati hiyo.

Kijiji cha Shenda wilayani Mbogwe mkoani Geita hakina Zahanati kwa zaidi ya miaka 20 tangu kianzishwe hali inayowalazimu kufasiri umbali wa kilometa nne kupata huduma za afya.

MATUKIO KATIKA PICHA:

 WANAWAKE WA KIJIJI CHA SHENDA WAKIWA NA NDOO WAKISOMBA MAJI,KOKOTO NA MCHANGA KATIKA UJENZI HUO.

 WANANCHI WA KIJIJI CHA SHENDA WAKISOMBA MATOFALI KUPELEKA ENEO LA UJENZI.

 MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA MBOGWE ELIUS KAYANDABILA KUSHOTO AKISHIRIKIANA NA WANANCHI KUKATA NONDO NDOGO KWA AJILI YA KUTANDAZA KWENYE JAMVI.

 MWONEKANO WA JENGO LA ZAHANATI INAYOJENGWA KATIKA KIJIJI CHA SHENDA.

 MAFUNDI WAKIFUNGA MBAO KWA AJILI YA KUMWAGA ZEGE KWENYE JAMVI .

 MKUU WA WILAYA YA MBOGWE BI MARTHA MKUPASI ALIYESIMAMA AKIWAELEKEZA WANANCHI NAMNA YA KUPANGA MAWE KUINUA NONDO.

 WANANCHI KWA KUSHIRIKIANA NA MKUU WA WILAYA WAKISUKA NONDO KWA AJILI YA KUMWAGA JAMVI.

 KAZI IKIENDELEA KATIKA UZINDUZI WA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA SHENDA.

KINA MAMA WAKISOMBA MAJI KUMWAGIA UKUTA KABLA YA KUMWAGA ZEGE.

 WANANCHI KWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA VYAMA NA MKUU WA WILAYA WAKICHANGANYA ZEGE.

 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MBOGWE ELIUS KAYANDABILA KUSHOTO AKICHANGANYA ZEGE NA WANANCHI.

 WANANCHI WAKIWA WAMEJIPANGA NA VIONGOZI WAKISOMBA ZEGE KWA AJILI YA KUMWAGA KWENYE MSINGI WA ZAHANATI.

 MAFUNDI WAKIENDELEA KUSUKA NONDO ILI WAWEZE KUMWAGA ZEGE.

 MKURUGEZBI AKIWA AMEJIPANGA KWENYE FOLENI KUPOKEA ZEGE NA KUMWAGA KWENYE MSINGI WA ZAHANATI.

 MKUU WA WILAYA YA MBOGWE BI MARTHA MKUPASI AKIONGEA NA WANANCHI MARA BAADA YA KUMALIZA KUZINDUA UJENZI WA ZAHANATI.

 WANANCHI WA KIJIJI CHA SHENDA WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MKUU WA WILAYA HIYO HAYUPO PICHANI.

 MKUU WA WILAYA YA MBOGWE BI MARTHA MKUPASI AKISAINI KITABU CHA WAGENI
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MBOGWE ELIUS KAYANDABILA AKIELEZEA MIPANGO YA HALMASHAURI KATIKA KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI HIYO.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata