DC KAHAMA AMPONGEZA BAKUNGILE KUANZISHA CHUO CHA AFYA,AWATAKA WAFANYABIASHARA WENGINE KUIGA MFANO HUO.


SERIKALI Wilayani Kahama imewataka wafanyabiashara kufikiria uwezekano wa kujenga vyuo vingi wilayani humo kama njia moja wapo ya kukuza uchumi na kuongeza ajira.

Akizungumza jana kwenye Mahafali ya Kkwanza ya Chuo cha Sayansi ya Afya Kahama yaliyoambatana na Uzinduzi wa chuo hicho, Mkuu wa Wilaya hiyo, FADHILI NKURLU amewataka wafanyabishara kuiga mfano wa Mfanyabiashara YONAH BAKUNGILE ambaye ni mmiliki wa Chuo hicho.

NKURLU amesema kuwa ikiwa wafanyabiashara watafanya hivyo watakuwa wameunga mkono jitihada za Rais JOHN MAGUFULI za kuijenga Tanzania ya Viwanda kwani azma hiyo haiwezi kufikiwa bila kuwa na wataalamu wa fani mbalimbali.

Kwa upande wake, mmiliki wa chuo hicho YONAH BAKUNGILE amewataka wafanyabiashara kutafuta fursa ya kuwekeza vyuo kwani Watanzania wengi wanahitaji kupata taaluma na  kwamba hali hiyo itasaidia Watanzania kupata taaluma ndani ya nchi badala ya kutegemea vyuo vya nje.

 


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata