CHAMA CHA CHAKAMWATA CHASAMBARATIKA MKOANI SHINYANGA,KATIBU WAKE AKABIDHI NYARAKA ZOTE CWT.

MWALIMU LAWRENCE MBAGA KUSHOTO AKIKABIDHI NYARAKA ZA CHAMA CHA CHAKAMWATA KWA UONGOZI WA CWT WILAYA YA KAHAMA.


 KAHAMA

CHAMA cha walimu mkoa wa Shinyanga CWT kimewataka viongozi wa chama hicho katika wilaya zote za mkoa huo kufanya kazi kwa ufanisi na kupuuza utitiri wa vyama vipya vinavyoanzishwa vyenye kujinasibu kuwasaidia walimu nchini.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu mkoa wa Shinyanga George Nyangusu kufuatia aliyekuwa katibu wa Chama cha CHAKAMWATA mkoa wa Shinyanga Mwalimu Lawrence Mbaga Kutangaza kujiondoa kwenye chama hicho na kukabidhi nyaraka zote kwa uongozi wa CWT Wilaya.

Nyagusu amesema kuwa Chama cha walimu Tanzania CWT bado kipo imara na kwamba walioanzisha chama cha CHAKAMWATA  ni wale waliokosa uongozi ndani ya CWT katika chaguzi zilizopita na kwamba chama hicho hakina malengo chanya ya kuwasaidia Walimu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Wilaya ya Kahama Edina Kalambo amempongeza Mwalimu aliyeamua kujitoa katika chama cha CHAKAMWATA na kutoa wito kwa walimu kuwa wamoja wanapopigania haki zao kuliko kujigawa.

Kalambo ameongeza kuwa kusambaratika kwa Chama hicho mkoani Shinyanga na Wilayani Kahama kumekuwa ni tuzo kwake ukizingatia kuwa amechaguliwa hivi karibuni Kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Walimu CWT wilayani Kahama.

Akielezea hatua ya Kusambaratika kwa Chama Hicho wilayani Kahama Katibu wa CWT wilayani Kahama Dauda Bilikesi amesema kuwa kwao ni faraja kwani chama hicho kilianza kutishia mshikamo  wa Walimu ila kwasasa walimuwatarudi katika umoja wao na kwamba CWT inatosha kutetea maslahi ya walimu pasipo kuwa na vyama vingi Nchini.

Akielezea sababu za kujitoa aliyekuwa Katibu wa Chama cha Kutetea Haki na masilahi ya walimu Tanzania (CHAKAMWATA) Lawrnce Mbaga amesema kuwa ameamua kujitoa kwasasabu Viongozi wa chama hicho Hawapambani na changamoto za Walimu bali wanapambana na Chama cha Walimu Tanzania CWT.

Sambamba na hayo Mbaga ameongeza kuwa Chama hicho kimemfanya atumie pesa nyingi za Familia kukiendesha  ikiwa ni pamoja na kuwataka walimu wote aliowaunganisa katika chama hicho kukipuuza chama hicho na kusema kuwa uongozi aliouunda katika kata zote ameuvunja na haupo tena.
 VIONGOZI WA CWT WILAYA YA KAHAMA WAKIMPONGEZA MWALIMU MBAGA BAADA YA KUTANGAZA KUACHANA NA CHAMA HICHO NA KUVUNJA UONGOZI ALIOKUWA AMEUWEKA.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata