CHADEMA KUTOA BIMA ZA AFYA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa kitabadilisha fikra za wananchi pamoja na mazoea ya kwenda hospitali pale wanapokuwa wanaumwa na badala yake watawajengea uwezo wa kwenda hospitali mara kwa mara ili kujua Afya zao.

Hayo yamesemwa na Katibu wa CHADEMA Dar es salam na Mjumbe Baraza kuu na Mkutano Mkuu Taifa Henry Kilewo ambaye amesema pamoja na kuwajengea uwezo wananchi watatoa na bima za afya kwa wananchi.

"Chadema tutakapokuwa Tunaongoza Nchi 2020 tutabadili Fikra za Mazoea Kwa Wananchi kusubiri Kuumwa ndiyo waende Hospital,Tutawajengea Uwezo wa Kucheki Afya Zao Mara kwa Mara pamoja na kuwapatia Bima za Afya" Kilewo.

Mbali na hayo Kilewo amefafanua kwamba ni muda muafaka kwa serikali kuwekeza kwenye Sekta ya Afya mahali ambapo panadaiwa kuwa na changamoto huku akikosoa namna Tanzania ilivyo nyuma kwenye sekta ya afya.

"Ni aibu na dhihaka kwa Taifa kwa watu kujazana kwenda kupata matibabu kwenye meli ya wachina, hii inaonyesha ni namna gani tulivyo nyuma kwenye Sekta ya Afya...Viongozi wetu kama wanashabikia hili basi Taifa lipo kwenye msiba mkubwa wa uongozi,Taifa linalia". Ameandika Kilewo kwenye ukurasa wake wa Twitter

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata