BILIONEA DR LOUIS SHIKA ATUA KAHAMA,AHIDI KUTOA BILIONI MBILI KUSOMESHA WATOTO YATIMA KILA MWAKA. DR LOUIS SHIKA AKITOA NENO KATIKA MAHAFALI.
 
KAHAMA
SERIKALI Wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeshauriwa kuomba msaada kusomesha watoto yatima na wasiyo na uwezo kutoka kwa kwa Bilionea aliyetaka kununua nyumba za mnada za Lugumi Dr Louis Shika ili kuinua kiwango cha elimu na kutoa elimu kwa makundi yote wilayani humo.


Wito huo umetolewa leo mjini Kahama na Bilionea huyo Dr Shika katika mahafali ya Kwanza na uzinduzi wa chuo cha Sayansi ya Tiba (Kahama College of Health and science) wakati akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa chuo hicho kumkaribisha kuwa mgeni wa muhimu katika mahafali na uzinduzi wa chuo hicho.
Dr Shika amesema kuwa yeye ni Mpenzi wa elimu na anapenda watu wote wapate elimu hivyo kupitia kampuni yake ya Lancefort atasaidia kusomesha wanachuo ambao wazazi wao wameshindwa kuwalipia ada na wale ambao ni yatima wazazi wao wamefariki.

Hatua hiyo imekuja kufuatia Risala ya chuo hicho iliyosomwa na Mkuu wa Chuo hicho na kuelezea changamoto wanazokutana nazo kuwa ni pamoja na wazazi kushindwa kulipa ada pamoja na waanachuo wengine kushindwa kuhitimu mafunzo yao baada ya wazazi wao kufariki.

Sambamba na hayo Dr Shika ametoa wito kwa Ofisi ya mkuu wa wilaya imuombe kusaidia kusomesha wanafunzi wasio na uwezo kwani kampuni yake inauwezo wa kusaidia watoto yatima katika wilaya ya Kahama hivyo milango iko wazi na yeye yuko tayari kusaidia watu wenye njaa ya Elimu.

Akielezea kiwango atakachokitoa kusomesha wanachuo hao Dr Shika amesema kuwa itakuwa ni dola milioni moja za Kimarekani sawa na Bilioni mbili ambazo atakuwa anazitoa kila mwaka kwa chuo hicho kwa ajiliya kuwasaidia wanafunzi wanaopenda kusoma ila wanashindwa kutokana na ukosefu wa ada.

Katika hatua nyingine Dr Shika amesema kuwa waandishi wa habari na mwenyechuo wasimuulize kuhusu msaada huo ndani ya wiki mbili kwani kwasasa hana pesa bali wasubiri mpaka mchakato wake wa kuhamisha fedha zake kutoka Urusi ukamilike.

Nae mkurugenzi wa chuo hicho  YONAH BAKUNGILE amesema kuwa  kumekuwa na shida ya wanafunzi wanaomaliza vyuo  vya uuguzi kutokuwa na maadili na kufikilia masirahi jambo ambalo limechangia kupoteza maana halisi ya masomo hayo.

Amewataka kuitumikia jamii bila kuangalia masrahi na kuwahudumia watui walionacha na wasiokuwa nacho  ikiwa ni kutimiza malengo  na nia ya kuanzisha vyuo vya uuguzi katika kuihudumia jamii katika maeneo mbali hapa nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali hayo amemwelezea Dr Shika kuwa ni mtu wa pekee mwenye utulivu na usikivu na kuongeza kuwa wadau wengine waige kama alichofanya Dr Shika katika kuinua Elimu Nchini.

MATUKIO KATIKA PICHA:
MKUU WA WILAYA YA KAHAMA MH FADHILI NKULU MWENYE JOHO NA MIWANI NYEUSI AKIWA KATIKA MOJA YA CHUMBA CHA KUFUNDISHIA KATIKA CHUO HICHO.

 

WAHITIMU WA WAKIWA WAMESIMAMA KUMPOKEA MGENI RASMI
 

WANACHUO WANAOBAKI WA MWAKA WA KWANZA NA MWAKA WA PILI WAKIWA WAMEKETI  KATIKA NAFASI ZAO.
 

BAADHI YA WAZAZI WALIOHUDHURIA KATIKA MAHAFALI HAYO WAKIWA KATIKA NAFASI ZAO.
KIKUNDI CHA SANAA KUTOKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA KIKITUMBUIZA KATIKA MAHAFALI HAYO

MKURUGENZI WA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA MR YONAH BAKUNGILE AKITOA NENO KWA WAHITIMU.

DR SHIKA AKIPEANA MKONO NA MKUU WA WILAYA YA KAHAMA FADHILI NKULU BAADA YA KUMALIZA KUTOA NENO.

DR SHIKA AKIPEANA MKONO NA MKURUGENZI WA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA MR YONAH BAKUNGILE
DR SHIKA AKIENDELEA KUPEANA MKONO NA VIONGOZI WALIOKUWA MEZA KUU

BAADHI YA WAFANYA BIASHARA WA MJINI KAHAMA WAKIWA WAMETULIA KATIKA MAHAFALI KUMSAPOTI MFANYABIASHARA MWENZAO

DR SHIA AKIHITIMISHA KWA KUSEMA MSEMO WAKE WA 900 ITAPENDEZA.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata