BAADA YA MNUNUZI WA TUMBAKU KUPATIKANA MWENYEKITI KACU AWAPONGEZA WAKULIMA KWA UVUMILIVU.

MWENYEKITI WA KACU EMMANUEL CHEREHANI.
KAHAMA:
Wakulima wa Tumbaku katika halamshauri ya Ushetu Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameupongeza uongozi wa KACU na serikali kwa ujumla katika kufanikisha mpango wa kununua tumbaku zilizokuwa zimebaki kwa wakulima ambazo zilizalishwa nje ya makisio.

Wakizungumza na Kijukuu Blog wananchi hao wamesema KACU na serikali wamefanya juhudi kutafuta masoko kwaajili ya kununua tumbaku iliyokuwa imebaki kwa wakulima licha ya hasara waliyopata  baada ya tumbaku kushindwa kununuliwa kwa wakati.

Wamesema kuwa kutokana na kuchelewa kununuliwa kwa tumbaku zao imesababisha kuchelewa kupata pesa kwaajili ya kununua chakula na matumizi mengine ikiwemo kupeleka watoto shule kutokana na kwamba wakulima wengi wanategemea zao la tumbaku kama zao la biashara .

Nae Masolwa Donald mkazi wa ulowa no.3 ameipongeza serikali kupata mnunuzi wa tumbaku zao ambapo ameiomba serikali na uongozi wa KACU kuongeza juhudi ya kutafuta wanunuzi wengi watakao weza kunua tumbaku nyingi kulingana na uzalishaji wa wakulima.

Kwaupande wake mwenyekiti wa Kacu Emanuel Cherehani kwanza amewapongeza wakulima wake kwa uvumilivu licha ya adha walizopata ,ambapo amesema KACU ,wanunuzi na Serikali wamkubaliana kununua tumbaku iliyobaki na kwamba soko litaanza tarehe 24 novemba mwaka huu.

Hata hivyo Cherehani amewataka wakulima kuzingatia utaratibu bila kuweka uchafu kwenye mitumba ili soko liende kama lilivyo pangwa kwani mnunuzi ametoa siku 20 za kununua tumbaku hizo,ambapo bei ya ni wadolla 1.5 kwa tumbaku ya kawaida .

Ameongeza kuwa kwasasa wamefanya makisio na kutoa maelekezo kwa viongozi wa vyama vya msingi kusimamia makadirio ya tumbaku itakayozalishwa kwa msimu huu ili kuondoa usumbufu kama ulivyo jitokeza msimu uliopta wa kubakiza tumbaku ya ziada. Kwa wakulima.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata