ASKARI MGAMBO KAHAMA WACHANGIA UNIT 85 ZA DAMU,HUKU WANANCHI WAKISHAURIWA KUCHANGIA DAMU.



 Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameshauriwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangia damu ili kuokoa vifo  vya akinamama wajawazito, watoto na watu wanaopata ajali.

Ushauri huo umetolewa leo  na Kaimu mkuu wa kitengo cha Maabara katika hospitali ya mji wa Kahama, GETRUDA GOMBA wakati akizungumza na Kijukuu Blog, ambapo amesema  hospitali hiyo bado inauhitaji  wa damu kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa.

Ili kumudu mahitaji ya wagonjwa wanaohitaji damu, Hospitali ya Mji wa Kahama inahitaji uniti  20 kwa siku, sawa na unit 560  kwa mwezi, kwani kwa sasa wanafikia uniti 15 kwa siku sawa na uniti 252 kwa mwezi.

GOMBA amesema  katika kipindi cha mwezi Julai  hadi  septemba mwaka huu, Mwanamke mmoja alifariki dunia wakati akijifungua kutokana na kukosa damu.

Katika hatua nyingine, GOMBA amewashukuru askari wa Jeshi la Akiba (Mgambo) wilayani Kahama kwa kuchangia jumla ya uniti  85 katika Kitengo hicho.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata