ALIYEFARIKI MIEZI 6 ILIYOPITA AFUFUKA NA KUONEKANA MTAANI IGOMA MWANZA

Mwanamke Chausiku Miligo aliyedaiwa kufariki na kuzikwa miezi sita iliyopita, amezua taharuki kubwa baada ya kuonekana tena mtaani kwake Mbugani Kata ya Igoma, jijini Mwanza akiwa hai.

Majirani wa mwanamke huyo wameshangazwa na kitendo cha yeye kuonekana huku wakipigwa taharuki, kwani walithibitisha kifo chake na hata kuzikwa kwake.

Chausiku alipoulizwa mahali alipokuwa katika kipindi chote cha miezi sita alieleza kwamba alikuwa wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu ambapo amemuacha mtoto wake wa kiume.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbugani aalieleza kuwa Chausiku aliugua ghafla akiwa mjamzito na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Seketule ambapo baada ya muda mfupi alifariki dunia na kisha taratibu za maziko zikafuatwa.

“Huyu mama aliugua na hatimaye akapelekwa katika hospitali ya mkoa ya Seketule, na baadae tulipata taarifa kuwa amefariki dunia na sisi kama mtaa tulifuata taratibu zote za kumsitiri. utaratibu wa maziko ulifanyika Shinyanga. Kwa hiyo tuliuaga na kutoa heshima zetu za mwisho na huyu mama alisafirishwa akapelekwa kuzikwa shinyanga,” alisema mwenyekiti wa mtaa wa Mbugani.

Umati wa watu ulikusanyika kushuhudia tukio hilo la aina yake ambapo kila mmoja alibaki akishangazwa kwa tukio hilo.

Familia ya Chausiku imeeleza kuwa ina mpango wa kumfanyia tambiko ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata