AKAMATWA KWA KUUZA SILAHA YA ASKARI MWENZAKE

Askari ambaye ni miongoni mwa wanaosindikiza msafara wa rais (Body guards) amepandishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili za kuuza silaha ya askari mwenzake.

Mtuhumiwa huyo wa kambi ya Ruiru nchini Kenya alikamatwa Jumamosi hii akiwa katika harakati za kuuza silaha hiyo aina ya Jericho yenye risasi 15 kwa mtu ambaye anaaminiwa ni jambazi katika eneo la Kawangware.

Askari ambao walikuwa zamu walipata taarifa kutoka kwa raia wema na kumfuatilia mwenzao huyo, na ndipo walipomkamata akiwa kwenye harakati za kuuza na kuichukua silaha hiyo.

Askari huyo pia anatuhumiwa kuhusika na kukodisha silaha za moto kwa wahalifu.

Citizen

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata