WANAOPITILIZA MUDA WA KULIPIA FAINI YA MAGARI BARABARANI KUKIONA

Kikosi cha usalama barabarani nchini kimefanikiwa kukamata zaidi ya magari 2000 jijini Dar es salaam baada ya kuja na mfumo mpya wa kukamata magari ambayo yanazidisha muda wa kulipiwa faini baada ya kukamatwa na makosa mbalimbali.

Mfumo huo unaotambulika kama (TMS Check) au Mfumo wa kufuatilia makosa ya usalama barabarani umeanza kutumika Septemba 28.

Akizungumza leo Afisa usalama makao makuu ya Kikosi cha usalama barabarani PC David amesema kuwa mfumo huo umeonesha mafanikio makubwa tangu uanze kutumika kubaini wamiliki wa magari wanaochelewa kulipa faini baada ya kukamatwa.

“Mfumo huu umeanza kufanya kazi tangu Septemba 28 ambapo umefanikisha kukamatwa kwa magari zaidi ya 2000 jijini Dar es salaam ya watu wanaokamatwa na makosa kisha kupitiliza muda wa kulipa faini zao”, amesema PC David.

Aidha PC David amefafanua kuwa mfumo huo unamwezesha askari wa usalama barabarani kulitambua gari linalodaiwa, kupitia simu maalum ambayo gari likikaribia inaingizwa namba ya gari kisha simu inatoa majibu endapo gari linadaiwa au halidaiwi.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata