WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NYASUBI KAHAMA,WAIOMBA SERIKALI KUWABANA WATU WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI.Serikali imeshauriwa kuendelea kuweka mkazo kwenye sheria zinazowakuta na hatia watu wanaowapa mimba wanafunzi wa kike,  pamoja na jamii kuwa mstari wa mbele kuwalinda watoto wa kike  dhidi ya vikwazo.

Hayo yamesemwa na  baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyasubi wakati wakizungumza na Kijukuu Blog, ikiwa leo ni siku ya Mtoto wa Kike dunia ambapo pia wameomba kuboreshewa miundombinu ya shule.

Wanafunzi Hao MIZA CHARLES, ZUENA JUMA, PAULINA  EDWARD wamesema   njia hiyo itasaidia kutoa nafasi kubwa kwa watoto wa kike kufikia malengo yao hasa katika sekta ya Elimu.

Nao baadhi ya walimu wa Kike wa shule hiyo wameiomba jamii kuwaendeleza kielimu watoto wa kike kwani wanahaki sawa na watoto wa kiume katika kupata haki hiyo.

Siku ya mtoto wa Kike Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Oktoba 11 na mwaka huu kitaifa imefanyika mkoani Mara, ikiwa na kauli mbiu isemayo “Tokomeza mimba za utotoni tufikie uchumi wa viwanda”.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata