WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI KWEMA YA MJINI KAHAMA WAWATOA JASHO WALIMU WAO KIMICHEZO.

WANAFUNZI WA SEKONDARI YA KWEMA WAKIWA NA WALIMU WAO KATIKA MAJIBIZANO YA KUSHANGILIA WAKATI MECHI YA MPIRA WA MIGUU IKIENDELEA.
 KAHAMA
Wanafunzi  wa Kwema Modern Secondary school wameonesha umwamba dhidi ya walimu na watumishi wa shule hiyo katika mechi  za uzinduzi wa viwanja vya michezo vya shule hiyo.


Katika mchezo wa kwanza timu ya mpira wa miguu ya wanafuzni wa shule hiyo walikuwa wakwanza kupata gori la kwanza kupitia kwa mshambuliaje wake Samweli Musa.


Katika kipindi cha pili walimu wa shule hiyo walifanikiwa kurudisha gori hilo kupitia kwa mchezaji wao Emmanuel Maiko.


Hadi dakika za mwisho za kipenga cha refa kinapulizwa matokeo yalikuwa moja kwa moja.

Katika hatua nyingine mpuliza kipenga akaweka matuta ya penati ambapo timu zote zilifungana bao 5 kwa 5.


Katika matuta ya piga nikupige timu zote zilifungana bao mbili kwa mbili na makapteni kuamua mchezo uishe kwa droo.


Akizungumza na Kijukuu Blog Captain wa timu ya wanafunzi wa Kwema Modern Secondary School mara baada ya mechi kuisha amesema kua mchezo walioutegemea umekua tofauti na mategemeo kwani walidhani walimu wao wazembe ila haikuwa hivyo. 


Kwauapande wake kocha wa timu ya walimu Mwalimu kazimoto amesema kuwa alitegema matoke makubwa lakini kujipanga kwa wanafunzi wao  ameyapokea matokeo hayo kama yalivyotokea.


Katika mchezo wa pili  wa mpira wa pete timu ya wasichana ya wanafunzi  imewafunga walimu wao magori manane kwa mawili huku watumishi wakijinasibu kuwa umri ndiyo tatizo pamoja na kutofanyamazoezi kumechangia kufungwa.


Walimu,Watumishi pamoja na wanafunzi wameushukuru uongozi wa shule hiyo kwa kuanzisha viwanja vya michezo na kununua vifaa vya kutosha vya michezo zikiwemo jezi,mipira na vifaa tiba na kwamba hatua hiyo itasadia kufanya mazoezi mara kwa mara shuleni hapo.

MATUKIO KATIKA PICHA:

 DAWATI LA UFUNDI LA TIMU YA MAVETERANI YA WATUMISHI WA SHULE YA SEKONDARI YA KWEMA WAKIFUATILIA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU 

 MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU UKIENDELEA KATI YA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA KWEMA NA WALIMU WAO.

 WANAFUNZI WAKIWA NA WALIMU WAO NJE YA BENCHI WAKIFUATILIA MCHEZO HUO.

 WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA NA CHA NNE WAKIWA NJE YA UWANJA KUWASHANGILIA WENZAO.

 KIONGOZI WA TIMU MAVETERANI YA WATUMISHI WA KWEMA SEKNDARI AKIWA NA WANAFUNZI WAKIFUATILIA MCHEZO HUO.

 WANAFUNZI WAKIWA KATIKA NYUSO ZA FURAHA BAADA YA WENZAO KUSHINDA GORI LA KWANZA DHIDI YA WALIMU WAO.

 WANAFUNZI WAKIWA NA SHANGWE ZA KUTOSHA BAADA YA KUONGOZA KWA GORI LA KWANZA.

 NI MWENDO WA SHANGWE KWAKWENDA MBELA HAKIKA USHINDI NI MTAAMU.

 WANAFUNZI WA MASOMO YA SAYANSI WANAOSOMA KATIKA SHULE HIYO WAKIWA KATIKA KITENGO CHA HUDUMA YA KWANZA KATIKA MICHEZO HIYO.

 MWANDISHI WA HABARI WA KIJUKUU BLOG ALAN KABASELE AKIFANYA MAHOJIANO NA MSHABIKI WA TIMU YA MAVETERANI YA WATUMISHI WA KWEMA.

 VIJANA WAKIENDELEA KUMENYANA NA WALIMU WAO KATIKA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU.

 GORIKIPA WA TIMU YA WALIMU AKIJITAHIDI KUOBNDOA MPIRA KWENYE ENEO LA HATARI.
 
WATU WA HUDUMA YA KWANZA WAKIKIMBIA UWANJANI KUTOA MATIBABU YA MCHEZAJI ALIYEUMIA.

 WATU WA HUDUMA YA KWANZA WAKIMTOA NJE MCHEZAJI AMBAYE ALIUMIZWA UWANJANI KATIKA MCHEZO HUO.

 WATU WA HUDUMA YA KWANZA WAKITOA MATIBABU.

 MOJA KATI YA HUDUMA NZURI YA SHULE ZA KWEMA NI MATIBABU,AMBAPO HII NI GARI ILIYOKUWA UWANJANI KWA AJILI YA KUTOA HUDUMA ENDAPO MCHEZAJI AU MTU YEYOTE ATAPATA MATATIZO KATIKA ENEO HILO.

 MARA BAADA YA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU KUMALIZIKA WANAFUNZI PAMOJA NA WALIMU WALIHAMIA KATIKA MCHEZO WA MPIRA WA PETE.

 UBAO WA MATANGAZO ULIOBEBWA NA MMOJA WA WANAFUNZI UKIONYESHA MATOKEO MARA BAADA YA DAKIKA 90 ZA MCHEZO HUO KUMALIZIKA.

 WANAFUNZI WAKIWA WAMETULIA KUSHUHUDIA PENATI KATI YA WANAFUNZI NA WALIMU WAO.

 KIKOSI CHA TIMU YA MAVETERANI WATUMISHI WA KWEMA WAKIJIPANGA NANI NA NANI WAPIGE PENATI.

 TIMU YA WANAFUZNI NAO WAKIJIANDAA KUCHAGUA WATU GANI WA KUPIGA PENATI.
 
 GORIKPA WA TIMU YA WALIMU AKIA HAAMINI KILICHOTOKEA BAADA YA KUFUNGA PENATI YA TATU.

 MWANDISHI WA KIJUKUU BLOG ALAN KABASELE AKIFABNYA MAHOJIANO NA KAPTENI WA TIMU YA WANAFUNZI MARA BAADA YA MPIRA KUMALIZIKA.

 MPIRA WA PETE KATI YA WANAFUNZI NA WALIMU NAPO UKASHIKA KASI AMBAPO WANAFUNZI WALIWAFUNGA WALIMU MAGORI MANANE KWA MAWILI.

 VUTA NIKUVUTE KATIKA MPIRA WA PETE IKIENDELEA.
 
 WALIMU NA WAFANYAKAZI WA KIUME WA SHULE YA KWEMA WAKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUWASHANGILIA WALIMU WA KIKE WAKATI MCHEZO WA MPIRA WA PETE UKIENDELEA.

 GARI LA WAGONJWA LA HOSPITALI YA KWEMA LIKIWA UWANJANI KUMBEBA MWANAFUNZI AMBAYE ALIPATA MATATIZO YA MIGUU WAKATI AKICHEZA.

 DEREVA WA GARI LA WAGONJWA AKIMUWAHISHA HOSPITALI MWANAFUNZI ALIYEUMIA MGUU AKIWA MNCHEZONI.

 WANAFUNZI NA WALIMU WAKISHANGILIA KWA PAMOJA MARA BAADA YA MCHEZO HUO KUMALIZIKA ISHARA YA MCHEZO WA KIRAFIKI.

 KARIBU KWEMA MODERN SECONDARY SCHOOL KWA MALEZI BORA NA ELIMU SAFI KWA MWANAO INAYOZINGATIA USALAMA,MICHEZO NA UFAULU MZURI.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata