WALIMU WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO KAHAMA,WAANDAMANA OFISI ZA AFISA ELIMU KUSHINIKIZA MKUU WA SHULE KUONDOLEWA BAADA YA KIFO CHA MWALIMU MWENZAO.


KAHAMA
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Nyihogo Halmashauri ya Mji wa Kahama GRACE KALINGA  (39) amefariki dunia muda  mfupi baada ya kudaiwa kujibishana maneno na Mkuu wa shule hiyo  ISMAIL ALLY.

Kwa mjibu wa walimu wa shule hiyo, Tukio hilo limetokea leo asubuhi majira ya saa tatu  baada ya mwalimu GRACE kwenda kwa mkuu wa shule hiyo kufuatilia ruhusa ya kwenda masomoni.

Hata hivyo walimu hao wameandamana hadi ofisi ya Afisa Elimu Sekondari ili kushinikiza  serikali imchukulie hatua za kinidhamu mkuu huyo kutokana na kifo hicho  ikiwa ni pamoja na kumuundoa katika shule hiyo.

Hata hivyo Taarifa zinasema kwamba walimu hao kwa sasa wanaendelea na Mazungumzo na katibu tawala wa wilaya ya Kahama TIMOTH NDANYA katika Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo ili kufikia mwafaka wa swala hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo ISMAIL ALY amesema hawezi kulizungumzia hilo kwa sasa kutokana na kuwa katika harakati za  Kupeleka taarifa  hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.

Mwili wa Marehemu mwalimu GRACE umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Mji wa Kahama huku Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dokta FREDRICK MALUNDE akithibitisha kupokea mwili huo.


 MATUKIO KATIKA PICHA:

 WALIMU WA SHULE YA SEKONDARI NYIHONGO WAKIWA BARABARANI KUELEKEA OFISI ZA AFISA ELIMU SEKONDARI HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

 WALIMU WAKIWA KWA MIGUU WAKIWA NJIANI ENEO LA BUKONDAMOYO KWENDA OFISI ZA AFISA ELIMU.
 MWALIMU EMMANUEL MAGEMA AKITOA MAELEZO MBELE YA MWANDISHI WA KIJUKUU BLOG NDALIKE SONDA KUHUSU TUKIO LILIVYOTOKEA NA MAAMUZI WALIYOFIKIA WALIMU.

 MWALIMU THERESIA MUSHI WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO AKIELEZEA TUKIO LA KIFO CHA MWALIMU MWEZAO KILIVYOTOKEA.

 MWALIMU THERESIA MUSHI AKIENDELEA KUELEZA SABABU ILIYOWAFANYA WAELEKEE OFISI ZA AFISA ELIMU SEKONDARI.

 WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO WAKIWA NJE YA MADARASA BAADA YA WALIMU KUTOINGIA DARASANI KUTOKANA NA TUKIO HILO.

 WALIMU WAKILIKARIBIA JENGO LA OFISI ZA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA KWA AJILI YA KUFIKISHA MALALAMIKO YAO KUHUSU TUKIO LILILOTOKEA SHULENI KWAO.

 WALIMU WAKIINGIA KATIKA OFISA ZA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

 WALIMU WAKIINGIA KATIKA OFISI ZA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

 WALIMU WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO WAKIWA MLANGONI WA AFISA ELIMU SEKONDARI HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

WALIMU WAKIMWELEZA JAMBO MMOJA WA MAAFISA WA HALMASHAURI WALIPOFIKA KATIKA OFISI HIZO.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata