WAKAZI WA NYASUBI WAMETAKIWA KUWA WAVUMILIVU KUHUSU UKOSEFU WA ZAHANATI.Wakazi wa Kata ya Nyasubi katika Halmashauri ya Mji wa Kahama ambao wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la ukosefu wa Zahanati wametakiwa kuwa wavumilivu wakati jitihada zinafanyika kukamilisha ujenzi wa Zahanati uliokuwa umesimama kwa muda mrefu.

Akizungumza na KIJUKUU BLOG kwa njia ya simu Diwani wa kata hiyo ABEL  SHIJA amesema ujenzi wa Zahanati  hiyo ulisimama kutokana na kesi iliyokuwepo mahakamani kati ya halimashauri ya mji wa Kahama na mmiliki wa eneo hilo CHRISTOPHER BUNDALA.

SHIJA ameongeza kuwa bajeti kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati hiyo imeshatengwa na kusisitiza kuwa ujenzi wa utaanza haraka iwezekanavyo, hivyo kuwaomba wakazi wa kata hiyo kutoa ushirikiano.

Katika hatua nyingine SHIJA amesema wananchi wanayo haki ya kuhoji kiasi cha pesa kilichotengwa katika miradi mbalimbali ya kata hiyo kwani ni haki yao ya msingi.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata