SAKATA LA KIFO CHA MWALIMU KAHAMA,WANAFUNZI NYIHOGO WAANDAMANA KUMTETEA MKUU WA SHULE,WATOA ORODHA YA WALIMU WANAOFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI. 
 BAADHI YA WANAFUZNI WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO WAKIWA KATIKA OFISI ZA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

KAHAMA
Wanafunzi zaidi ya 200 wa shule ya sekondari Nyihogo leo wameandamana hadi ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mji wa Kahama wakiishinikiza serikali isikubali kumwondoa mwalimu mkuu wa shule hiyo ISMAILY ALLY.

Maandamano hayo ya wanafunzi yamekuja  ikiwa ni siku tatu baada ya walimu wa shule hiyo  nao kufanya maandaano wakitaka serikali imuhamishe kituo cha kazi mwalimu huyo kwa madai ya amesababisha kifo cha mwalimu GRACE  OLIMBOKA aliyefariki dunia ghafla  siku hiyo.

Wakizungumza na KIJUKU BLOG  Baadhi ya wanafunzi wamesema  walimu mkuu amekuwa msatari wa mbele kuinua kiwango cha elimu shuleni  hapo na kwamba walimu wanaotaka ahamishwe ni wavivu wa kufundisha na baaadhi yao wametajwa kufanya mapenzi na wanafunzi wa kike.

Hata hivyo Katibu tawala wa wilaya ya Kahama TIMOTH NDANYA akizungumza na wanafunzi hao kwa naiba ya mkuu wa wilaya amesema vyombo vya dola vimeanza kufanya uchungunzi wa tuhuma zote  hivyo wanafunzi waendelee na masomo kama kawaida.

Hata hivyo Ndanya amesema mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya  wilaya ya Kahama FADHIL NKURLU na kamati yake watafanya mkutano leo saa nane mchana  shuleni hapo ikiwa ni njia ya kutatua mgogoro huo.

Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, ISMAILY ALLY amewataka wanafunzi kuendelea kumuombea marehemu GRACE na kwamba haki itatendeka  katika tuhuma anazotuhumiwa.

Ijumaa iliyopita walimu wa shule hiyo waliandamana hadi ofisi ya mkuu wa wilaya ya kahama wakishinikiza serikali imwondoe    mkuu wa shule hiyo wakimtuhumu kusababisha kifo cha mwalimu mwenzao aliyekuwa anafuatilia ruhusa ya kwenda masomoni.

MATUKIO KATIKA PICHA:

 MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ABEL SHIJA ALIYESHIKA KIPAZA SAUTI AKIONGEA NA WANAFUNZI KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI HIYO.

 BAADHI WA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO WAKIMSIKILIZA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA KAHAMA MJI (HAYUPO PICHANI)

 BAADHI YA WANAFUNZI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA MANEO YA MWENYEKITI WA HALMASHUARI YA MJI.

 MMOJA WA WANAFUNZI AMBAYE JINA LAKE HALIKUWEZA KUFAHAMIKA MARA MOJA,AKITOA MAELEZO KUHUSU KILICHOWAFANYA WAANDAMANE.

 MOJA YA BANGO AMBALO LILIBEBWA NA WANAFUZNI HAO 

 BAADHI YA VIONGOZI WA HALMASHAURI WALIOJITOKEZA KUWASIKILIZA WANAFUNZI HAO,KULIA NI MWALIMU ALLY ISMAIL AMBAYE WANAFUNZI WANATAKA ASIONDOKE.

 WANAFUNZI WAKIONYESHA NYUSO ZA FURAHA BAADA YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA KUMKARIBISHA MWALIMU MKUU WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO AONGEE.

 MWALIMU MKUU WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO ALLY ISMAIL AKIONGEA NA WANAFUNZI KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI.

 BADHI YA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO WAKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI NJE YA UKUMBI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

 MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA AKIMKARIBISHA KATIBU TAWALA WA ILAYA BWANA TIMOTH NDANYA KWA KWA NIABA YA MKUU WA WILAYA KWA AJILI YA KUTOA MAAGIZO YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA.

 WANAFUNZI WAKIWA NJE YA UKUMBI WA HALMASHAURI BAADA YA KUAMBIWA WARUDI SHULENI.

 KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KAHAMA TIMOTH NDANYA AKIPANGA KWENYE GARI MARA BAADA YA KUMALIZA KUTOA MAAGIZO KWA NIABA YA MKUU WA WILAYA.
WANAFUNZI WAKITOKA KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI KUELEKEA SHULENI KWA AJILI YA KUSUBIRI KIKAO CHA ULINZI NA USALAMA.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata