RC SHINYANGA APIGA MARUFUKU KUKATA MTI BILA KIBALI.Serikali Mkoani Shinyanga imesema itachukua hatua kali kwa Mtu yeyote atakayebainika kukata  Miti bila ya Kuwa na Kibali Maalumu ili kutunza Mazingira.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ZAINAB TELLACK kwenye Hafla ya kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba yaliyofanyika Mjini Kahama.

Amesema atahakikisha kila wilaya Katika mkoa huo Inapanda Miti ili kukabiliana na mabadilko ya Tabia ya nchi ambayo yameanza kuteta athari katika Maeneo mbalimbali.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Misitu (TSF) Wilaya ya Kahama, BRUNO BAHANE amesema sheria ya Misitu ya mwaka 2002 kifungu namba 84 kinazuia Watu kuharibu Misitu bila Kibali.

Amefafanua kuwa kwa kipindi cha Mwezi agosti hadi Septemba jumla ya magari manne yameshakamatwa na kutozwa faini kwa kosa la kughushi vibali vya kusafirishia Mazao ya misitu na kuyapeleka katika Mgodi mdogo wa Mwime.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata