RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MASENETA KUTOKA MAREKANI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na Seneta James Inhofe pamoja na Maseneta wengine wa Baraza la Marekani Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Magufuli ameupokea ugeni huo na kufanya nao mazungumzo mbalimbali ndani ya Ikulu. Hata hivyo bado taarifa rasmi za nini haswa wameongea viongozi hao baada ya kukutana hazijatoka.
Pia leo Rais Dkt. John Pombe Magufuli amempokea kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu na kuteta mambo na mheshimiwa Rais.

Aidha Rais Dkt. Magufuli amepokea kitabu cha Seneta James Inhofe kilichoonyesha picha za maeneo mbalimbali ya Tanzania alipotembelea mwaka mmoja na nusu uliopita.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata