RAILA ODINGA AGOMA KUSAINI FOMU

Kiongozi wa Muunganiko wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA) Bwana Raila Odinga, amekataa kutia saini form 24A ambayo itamfanya awe amejitoa moja kwa moja kwenye uchaguzi wa Oktoba 26.

Odinga ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na moja ya kituo cha runinga nchini Kenya, na kusema kwamba anaendelea na msimamo wake wa kutoshiriki, lakini hatojaza form hizo.

Kauli hiyo imefuatia baada ya Tume huru ya Uchaguzi nchini humo IBEC, kusema kwamba ili kujitoa kwa Raila Odinga kuweze kukamilika, ni lazima ajaze form hiyo, la sivyo bado atabakia kuwa mgombea wa urais wa Oktoba 26.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa NASA Bwana Norman Mgaya, ameijibu tume hiyo akisema kwamba mahitaji ya mtu kujaza fomu ya 24A, haina mantiki katika uchaguzi huo.

Hivi sasa Raila Odnga yupo nchini Uingereza kwenye mkutano, huku akitarajiwa kuhutubia mkutano huo na kuelezea hali ya kisiasa ilivyo nchini Kenya.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata