OFISA TASAF: FREEMASON AIHUSIKI NA FEDHA ZA RUZUKU

Ofisa Ufuatiliaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) wilayani Biharamulo, Gerald Adolf amewataka wanufaika wa fedha za ruzuku zinazotolewa na mfuko huo kuepuka majungu kutoka kwa wasiowatakia mema wanaodai kuwa ni za kishirikina kutoka Freemason.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyabusozi, Adolf aliwataka wanufaika kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa kwa kutumia fedha wanazopata kupitia miradi yao ili Tasaf itakapomaliza muda wake waendelee kunufaika.

Mkazi wa kijiji hicho, Raulenti Kamoye alisema kutokana na fedha anazopokea amenufaika kwa kununua mashamba, kujenga nyumba bora, kuanzisha kilimo cha miti katika eneo la eka moja na kumiliki mifugo akiwa na mbuzi saba.

Mratibu wa Tasaf wilayani humo, Beatha Maganga alisema wamepokea Sh217.5 milioni kwa ajili ya kuwapatia walengwa waliopo kwenye kaya 6,969 kwa kipindi cha Julai hadi Septemba ili kuendeleza miradi waliyoanzisha kukabiliana na umaskini.

Beatha alisema kwamba fedha hizo zitagawiwa kwa wanufaika waliopo katika vijiji 11.

Mwananchi:

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata