MWENYEKITI MPYA WA CHAMA CHA WAKULIMA WA TUMBAKU MWADUI KAHAMA,AWAAHIDI MEMA WAKULIMA WAKE. MWENYEKITI WA CHAMA CHA MSINGI CHA WAKULIMA WA TUMBAKU MWADUI,EMMANUEL CHEREHANI.

KAHAMA

Wakulima wa zao la Tumbaku katika kijiji cha Mwadui Kata ya Ubagwe halmashauriya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kufuata maagizo ya wataalamu wa kilimo cha zao hilo ili kuleta tija na mafanikio katika msimu wa Kilimo 2017/2018.

Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti mpya wa chama cha msingi Mwadui Emmanuel Cherehani baada ya uchaguzi wa viongozi wa chama hicho uliofanyika jana kijijini hapo katika mwendelezo wa uchaguzi wa viongozi wa vyama vya msingi ulionza jana katika halmashauri ya ushetu.

Cherehani amesema kuwa kilimo cha Tumbaku kinahitaji elimu hivyo wakulima wa Tumbaku wanatakiwa kuwasikiliza wataalamu wa kilimo hususan katika kipindi cha ukuzaji wa miche ya tumbaku,Kupanda na kipindi cha kukausha.
Sambamba na hayo Cherehani amesema kuwa anatambua changamoto zinazowakabili wakulima wa chama cha msingi Mwadui na kwamba katika muda wake wa uongozi atahakikisha anazitatua ikiwa ni pamoja na kupigania masoko ya uhakika .

Katika uchaguzi huo uliokuwa na wagombea 9 na wapiga kura 179 Emmanuel Cherehani alipata kura 86,Huku aliyemfuatia akipata kura  19 ambaye ni Mihayo Mwita na kura 1 ikiharibika katika uchaguzi huo.

Wengine ni Lawrent Selemani aliyepata kura 14,Cosmas Mongela kura 26,Hussein Hamis Kura 5,Daud Pius kura 3,Richard Thomas kura 9,Philipo Seleman kura 15  na Bernard Michael kura 11.
 EMMANUEL CHEREHANI AMBAYE N MKULIMA WA TUMBAKU AKIWA KATIKA GHALA LA KUHIFADHIA TUMBAKU KATIKA KIJIJI CHA MWADUI.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata