MKURUGENZI WA SEKONDARI YA ANDERLEK KAHAMA AWATAKA WAZAZI KUWARITHISHA ELIMU WATOTO WAO KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA. MKURUGENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA ANDERLEK RIDGES,ALEXANDER KAZIMIL.

KAHAMA
Wazazi na walezi nchini, wameaswa kuwarithisha elimu watoto wao ili kuwa na taifa lenye wasomi wengi  na hivyo kufikia malengo ya  uchumi wa viwanda nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa  Shule ya Sekodnari ya Anderlek Ridges, ALEXANDER KAZIMIL katika mahafali ya 9 ya kidato cha nne yaliyofanyika leo Mjini Kahama.

Amesema ili  taifa na jamii iwe na mafanikio ya kiuchumi ni lazima wazazi na walezi wawekaze katika elimu ikiwa ni pamoja na kuzifahamu na kuzitatua changamoto zinawawakabili  wanafunzi wakati wa masomo na hatimaye wafikie malengo yao ya baadaye.

Meneja wa benki ya NMB, tawi la Kahama, RICHARD KIRENGA ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka wazazi kuwasaidia watato wao kuchagua masomo yatakayowaopatia ajira, badala ya kuwacha wajichagulie wenyewe hali inayoweza kuwakosesha ajira.

Jumla ya wanafunzi 138 wanatarajia kufanya mtihani yao ya mwisho ya Kidato cha Nne mwishoni mwa mwezi huu katika shule hiyo ya  Sekondari Anderlek Ridges,


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata