MKURUGENZI APANDISHWA MAHAKAMANI AKIWA KITANDANI

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Pwani (TAKUKURU) imemfikisha mahakamani aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Elimu Kibaha , Cyprian Mpenda kwa kosa la uhujumu uchumi huku akiwa amelala kitandani katika wodi namba 116 VIP Tumbi.

Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Sang'a amesema kuwa Mpemba anatuhumiwa kutokana na kosa la kutumia madaraka yake vibaya samba na uhujumu uchumi ambapo kati ya tarehe Agosti  6 mwaka jana katika Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani aliandaa na kusaini makubaliano kati ya Shirika la Elimu Kibaha na Kampuni ya CAGMT ambayo inamilikiwa na yeye mwenye na familia yake.

Kesi hiyo imesomwa mbele ya Mheshimiwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya kibaha Sofia Salum Masati. Aidha Mheshimiwa Hakimu Masati baada ya kusikiliza kesi hiyo amesema kuwa dhamana iko wazi huku mtuhumiwa Mpemba akitakiwa kuwa na wadhamini wawili huku kila mmoja akiweka dhamana ya  Sh. Mil.20

Mshtakiwa amekana shtaka hilo na kesi hiyo leo ndiyo imesomwa kwa mara ya kwanza itaendelea tena Mahakamani hapo ifikapo  Oktoba 25 mwaka huu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata