MKANDARASI KAMPUNI YA TINGWA COMPANY LTD ATAKIWA KUBOMOA MITARO ALIYOJENGA NYASUBI KAHAMA NA KUIJENGA UPYA KWA GHARAMA ZAKE. PICHA HII HAIHUSIANI NA TAARIFA.

Kamati ya ardhi, mipango miji na mazingira ya halmashauri ya mji wa kahama imemwagiza mkandarasi anayejenga mitaro ya barabara katika mtaa wa sango kata ya Nyasubi kuubomoa kutokana na kujengwa chini ya kiwango.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa kahama ABEL SHIJA amesema kamati hiyo imebaini mapungufu ya mkandarasi huyo, hivyo kumtaka abomoe na kuanza ujenzi upya kwa gharama zake.

SHIJA amesema kasoro nyingine ni mkandarasi aliyepewa tenda hiyo ambaye ni TINGWA COMPANY LTD kutokuwa eneo la kazi muda wote na kuwaachia vibarua ambao hawana uelewa wa kazi hiyo na kusababisha ubadhilifu wa fedha za serikali.

Akizungumza mbele ya kamati hiyo msimamizi wa ujenzi huo HAMISI KISIGO maarufu kwa jina la mzee MNGONI amesema mtaro huo haujajengwa tofauti na maelekezo ya halmashauri na kwamba amewasimamisha vijana wanaojenga mtaro huo ili waweze kurekebisha.

Ukarabati wa barabara ya Sango katika kata ya Nyasubi inayokarabatiwa kwa kiwango cha moram na mitaro ya maji pembeni ya barabara umetengewa bajeti ya shilingi milioni 76, na unatarajiwa kukamilika baada ya miezi mitatu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata