MIFUPA INAYODHANIWA KUWA YA BINADAMU YAKUTWA KWENYE BWAWA LILILOKAUKA LA TINDE - SHINYANGA


Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga ni kwama mifupa inayodaiwa kuwa ni ya binadamu imekutwa katika bwawa la Tinde. 
Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea leo mchana/jioni Jumatatu Oktoba 9,2017 wakati wananchi wakichimba kisima ndani ya bwawa hilo ambalo limekauka. 
“Walikuwa wanachimba kisima kwenye bwawa hili ambalo hivi sasa limekauka,wakati wanaendelea kuchimba ndiyo wakaona mifupa ya binadamu,hatujajua huyo mtu alifariki kwa njia gani,pengine alitumbukia kwenye bwawa wakati kuna maji ama alifukiwa na watu wasiojulikana”,kilieleza chanzo cha habari cha Malunde1 blog. 
Taarifa za awali zinasema Mkuu wa kituo cha polisi kituo cha Tinde pamoja na mbunge waViti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal wamefika eneo la tukio. 
Taarif zaidi tutawaletea hivi punde kupitia blog yako pendwa ya Malunde1 blog. 
Mwakilishi wa Malunde1 blog – Tinde,Said Nassoro ametutumia picha kutoka eneo la tukio,Tazama hapa chini
Mifupa inayodaiwa kuwa ni ya binadamu iliyokutwa kwenye bwawa la Tinde
Mifupa hiyo
Shimo ambamo kumekutwa mifupa
Wananchi wakishangaa
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal,mkuu wa kituo cha polisi Tinde na wananchi wakiwa eneo la tukio
Sehemu ya bwawa la Tinde likiwa limekauka
Bwawa likiwa limekaukaSAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata