MGOGORO WAWAFUGAJI NGORONGORO KUBAKI HISTORIA

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka wafugaji wa  Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kuwa watulivu wakati suala la mgogoro kati yao na hifadhi likiwa linashughulikiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Naibu Waziri Ulega ameeleza hayo jana katika mkutano na wafugaji hao uliofanyika kwenye Kata ya Ololosokwan wilayani humo.
Amesema Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli ni inawajali watu wanyonge hivyo wafugaji hao wavulimie na kwamba timu iliyoundwa na waziri mkuu siku za nyuma iliwashirikisha baadhi ya viongozi wao wakiwamo madiwani.
“Wakati tunamsubiri Waziri Mkuu atoe maelekezo naomba msiharibu hali ya hewa hii ndiyo rai yetu.Au kuna yeyote anayepinga jambo hili? Aliwauliza wafugaji hao na kujibiwa hakuna na wote wapo pamoja na Serikali.
“Hatua hii itaturahishishia sisi kwa sababu wizara inaliangalia jambo hili kwa ukaribu kutokana sehemu kubwa ya nchi wafugaji wamekuwa malalamiko makubwa sana ikiwamo kufilisia mifugo yao pindi inapoingia hifadhini na kusababishiwa umasikini,”amesema Ulega.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka alimweleza Ulega kwamba ukosefu wa malisho ni mojawapo ya changamoto inayowakabili wafugaji hao kutokana maeneo machache yaliyopo.
Hata hivyo, Ulega alihaidi kulishughulikia changamoto hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja watatafuta mashirika kwa ajili kuangalia namna ya kuboresha malisho hayo ili kuleta ahueni kwa wafugaji hayo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata