MBOWE AMPONGEZA RAIS MAGUFULI

Babati. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amepongeza kitendo cha Rais John Magufuli kuitenganisha Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwa kwa zaidi ya miaka saba kambi hiyo ilikuwa inaishauri Serikali kufanya hivyo.

Mbowe amesema hayo leo Jumamosi kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.

Amesema kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge zinaonyesha kuwa kambi rasmi ya upinzani ilikuwa inashauri wizara hiyo itenganishwe lakini ushauri wao haukufanyiwa kazi.

"Wizara ya Nishati na Madini ni wizara nyeti mno na mara nyingi tumekuwa tukiishauri Serikali iitenganishe wizara hiyo kwani ni kubwa na nyeti ila sasa wameona ushauri wetu unafaa na kuzitenganisha," amesema Mbowe.

Amesema suala siyo nani anafaa kuwa waziri na nani hafai kuwa waziri au ukubwa wa wizara ila suala ni kuona namna gani ya kuendesha Serikali ya Awamu ya Tano.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata