KINACHOENDELEA POLISI BAADA YA ZITTO KABWE KUKAMATWA

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, amekamatwa na polisi na kuhojiwa akituhumiwa kufanya makosa ya Uchochezi.
 
Kwamba juzi, Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo:
 
1. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.
 
2. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.
 
Timu ya mawakili wa chama iko na ndugu Zitto katika mahojiano haya.
 
Ado Shaibu - Katibu wa Itikadi, Mwasiliano ya Umma na Uenezi
ACT Wazalendo
Oktoba 31, 2017
Dar es salaam

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata