JERRY MURO ALIAMSHA DUDE KWA WABUNGE WA CHADEMA,AMTAKA LEMA ASEME WAKATI AKIWA NA RASTA ALIKUWA ANAFANYA NINI KABLA YA KUWA MBUNGE.

KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia aliwahi kuwa Msemaji wa klabu ya yanga, Jerry Muro ameibuka na kuwaponda viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku akiwataka waache porojo na badala yake wajikite katika kuwaletea maendeleo wananchi wao.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Muro amewataka viongozi wa Chadema wanaodai kuwa wanafuatiliwa na watu ili wauawe, waseme wanafuatiliwa na akina nani?

“Nimemsikia baadhi ya wabunge wa Chadema wakisema kuna watu wanawafuatilia, dada yangu kule Bunda (Ester Bulaya) akisema anafuatiliwa na watu waliovaa kininja, nani awafuatilie nyie? Kwani mmeiba makinikia?

“Lema naye anasema wamefungua nati za gari lake, pia anadai akiwa kwenye mwendokasi aliona watu wanamfuatilia akaruka kwenye gari akamwachia usukani mkewe, hivi kweli gari lipo kwenye mwendokasi unarukaje kichakani? Acheni maigizo jamani…” Nani akutafute wewe Lema? Mbona husemi wakati ukiwa na nywele za rasta ulikuwa unafanya nini kabla ya kuwa mbunge? alihoji Muro.

Ajibu kuhusu suala la madiwani wa Chadema Arusha waliohamia CCM, Muro amewataka Lema na Joshua Nassari waache kutembea na flshi (walizowasilisha TAKUKURU  kwa ajili ya uchunguzi) akidai kuwa hizo ni propaganda.

“Wakati Lema anazungumza na flashi Dar Es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo anahangaikia miradi ya maji na barabara kwa wananchi wake. Mimi namjua Lema tangu zamani, nimetoka naye Machame, aache kupambana na mimi Muro badala yake afanye maendeleo kwa wananchi wake.” alisema Muro.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata