JAGUAR AMUOMBA MSAMAHA BABU OWINO ILA AMTAKA KUMUHESHIMU RAIS

 Mbunge jimbo la Starehe jijini Nairobi Kenya kupitia chama cha Jubilee, Charles Njagua Kanyi maarufu kama Jaguar, ameomba msamaha kwa mbunge mwenzake kupitia NASA, Paul Ongili (Babu Owino), baada ya kupigana bungeni hapo jana.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika eneo la Bunge, Jaguar amesema kitendo hicho kilitokea kwa bahati mbaya, huku akiendelea kusisitiza kuwa mbunge huyo (Babu Owino) ni lazima aonyeshe heshima kwa Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta.


"Kilichotokea jana bungeni ni bahati mbaya, nakusamehe Babu Owino lakini pia namuomba anisamehe, hata hivyo nasisitiza kwamba Babu Owino lazima amuheshimu Rais, asipofanya hivyo nitashughulika naye", amesema Jaguar.


Hapo jana Mbunge Jaguar na Babu Owino walipigana wakiwa bungeni, baada ya Babu Owino kutamka maneno ya kumvunjia heshima Uhuru Kenyatta, kitendo kilichomchukiza Jaguar na kupelekea kukunjana bungeni na video zao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata