HIACE YAZAMA ZIWA VICTORIA NA KUUWA WATU 12.

Watu 12 wamekufa na wengine wameokolewa wakiwa salama baada ya Toyota Hiace kutumbukia Ziwa Victoria katika kivuko cha Kigongo Feri wilayani Misungwi.

“Kwa sasa uokoaji unaendelea, abiria kadhaa  ndio wametoka salama. Maiti nane zimeopolewa,” amesema Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Mkoa wa Mwanza, Ferdinand Mshama.Temesa ndiyo inasimamia kivuko hicho.

Mshama amesema gari hilo linafanya safari kati ya Buhongwa jijini Mwanza na kivukoni hapo.

Amesema ajali hiyo imetokea kutokana na gari hilo kupata hitilafu kwenye mfumo wa breki hivyo liligonga geti la kivuko na kutumbukia ziwani.

“Ni kweli gari limetumbukia, lilikuwa likitokea Buhongwa kupeleka abiria kivukoni, kabla dereva hajapaki lilifeli breki,” amesema na kwamba dereva alipita upande wa magari makubwa.
 

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata