HALMASHAURIYA KILWA YAJA NA MKAKATI KABAMBE WA KILIMO CHA KOROSHO,WAKULIMA SASA KUGAIWA MICHE BURE.

Mkakati wa serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu wa kuakikisha zao la korosho ambalo ni uchumi mkubwa wa wananchi wa mikoa ya kusini huenda likafanikiwa kwa hatua kubwa wilayani Kilwa Mkoani Lindi baada ya wilaya hiyo kuweka mkakati wa kupanda miche milioni moja kila mwaka na kuigawa bure kwa wakulima.

Hali hiyo imebainishwa jana na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo wakati wa ziara ya Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu George Kakunda wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani humo ambapo ametembelea vitalu vya kuzalisha mbegu ya korosho itakayogawiwa bure kwa wakulima.

Katika ziara hiyo Bugingo amesema tayari wameanza uzalishaji wa miche hiyo kwa hatua za awali na wilaya imeweka mikakati ya kupanda mbegu milioni moja kila mwaka wakati wakulima tangu zao hilo lianzishwe wanamiliki miti laki sita tu katika msimu uliopita wameweza kujipatia zaidi ya shilingi bilioni 13 wakati halmashauri imejipatia ushuru wa zaidi ya shilingi milioni 220 fedha ambazo ni kidogo kama mkakati huo wa kupanda miche milioni moja kila mwaka kama utakamilika.
 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KILWA ZABRON BUGINGO

Kwa upande wake Naibu waziri huyo amewataka viongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema miche hiyo inapandwa na kuota vizuri hali ambayo itaongeza pato kwa wananchi pamoja na uchumi wa Taifa na wao kama serikali watatoa ushirikiano kwenye eneo ambalo watahitajika.

Mbali na hali hiyo Waziri Kakunda ameupongeza mpango huo wa upandaji wa miche hiyo milioni moja kila mwaka kutokana na kuvuka malengo ya serikali ya kupanda miche elfu 50 kwa kila wilaya inayolima zao la korosho ingawa Afisa kilimo na ushirika wa halmashauri hiyo ya Kilwa John Mkinga amesema changamoto iliyopo ni ucheleweshwaji wa mbegu hali inayosababisha zoezi la uoteshaji miche hiyo kwenda taratibu ingawa Kakunda amesema atawasiliana na wizara ya kilimo kumaliza tatizo hilo.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata