DC KAHAMA AINGILIA KATI SAKATA LA NYIHOGO SEKONDARI,WALIMU WANAOFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI WAKALIA KUTI KAVU.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA,FADHILI NKULU AKIONGEA NA WANAFUNZI,WALIMU NA BODI YA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO.


KAHAMA

Mkuu wa wilaya ya Kahama FADHILI NKURLU  ametoa siku saba  kwa mkuu Upelelezi wilayani humo, akamilishe uchunguzi wa tuhuma  za kuhusishwa kufanya mapenzi na wanafunzi  wa kike wa shule ya sekondari Nyihogo zinazomkabili mwalimu mkuu hiyo pamoja na baadhi ya  mwalimu.

Akizungumza leo  baada ya kufanya ziara shuleni hapo amesema  tuhuma zilizotolewa na   wanafunzi dhidi ya baadhi ya walimu na zile zilizotolewa na walimu  dhidi ya mkuu wa shule hiyo zinafanyiwa kazi na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo.

Pia NKURLU ameseagiza shughuli za masomo ziendelee kama kawaida  na mkuu wa shule hiyo ISMALY ALLY na walimu wote waendelee kufundisha huku akiwataka wanafunzi kuendelea kuwa na nidhamu kwa walimu wote hivyo kuongeza  kiwango cha taaluma shuleni hapo.

Leo asubuhi Wanafunzi zaidi ya 200 wa shule  hiyo  wameandamana hadi ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mji wa Kahama wakiishinikiza serikali isikubali kumwondoa mwalimu mkuu wa shule hiyo ISMAILY ALLY.

Ijumaa iliyopita walimu wa shule hiyo waliandamana hadi ofisi ya mkuu wa wilaya ya kahama wakishinikiza serikali imwondoe mkuu wa shule hiyo wakimtuhumu kusababisha kifo cha mwalimu mwenzao aliyekuwa anafuatilia ruhusa ya kwenda masomoni.

MATUKIO KATIKA PICHA:

KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KAHAMA TIMOTH NDANYA AKIFANYA UTAMBULISHO WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WALIOMBATANA NA MKUU WA WILAYA KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO.

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOGO WAKISIKILIZA KWA MAKINI MAAMUZI YANAYOTOLEWA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA.

GEORGE BAGHEM AFISA WA JESHI LA POLISI MKUU WA UPELELEZI WILAYA AKIJITAMBULISHA MBELE YA WANAFUNZI NA BODI YA SHULE.

AFISA MAGEREZA AKIJITAMBULISHA MBELE YA WANAFUNZI NA BODI YA SHULE.

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ABEL SHIJA AKIJITAMBULISHA.

DIWANI WA KATA YA MUNGULA AKIJITAMBULISHA MBELE YA WANAFUNZI NA BODI YA SHULE.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA FADHILI NKULU AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI NA BODI YA SHULE KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA.

WALIMU WA SHULE YA SEKONDARI NYIHOO WAKIWA KATIKA KIKAO CHA KAMATI YAULINZI NA USALAMA KILICHOTEMBELEA KATIKA SHULE HIYO.

MKUU WA WILAYA AKIENDELEA KUZUNGUMZA NA WANAFUNZI,WALIMU NA BODI YA SHULE KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA,FADHILI NKULU MWENYE SUTI NYEUSI AKIWAPUNGIA MKONO WANAFUNZI MARA BAADA YA KUMALIZA KIKAO.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata