CCM YAMALIZA UCHAGUZI MASWA,PAUL NDUSHI JIDAYI APETA UWENYEKITI.

Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Maswa  Mkoani Simiyu kimepata Viongozi wake watakaokiongoza kwa kipindi kingine kijacho.

Uchaguzi huo umefanyika kwenye uwanja wa nguzo nane maswa ,Wanachama wa Chama hicho wamemchagua Eng. Paul  Ndushi Jidayi  kuwa  Mwenyekiti wa Chama wilaya kwa kupata kura 639 akimshinda Marco Jilala  Bukwimba aliyepata Kura 324  na Bi Grace  George Mbule  aliyepata kura 22 wapiga kura 988 huku tatu zikiharibika..

Wanachama pia waliwachagua Mayunga G Ngokolo kura 634, Jonathan Nandi kura 593 George Bugomela kwa kura 588, kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu taifa wa Ccm.

Wajumbe Mkutano Mkuu wa ( Ccm) Mkoa wamechaguliwa Boniface M  Ntungu  kwa kura 688 na Nzingula  N Nyuta kura 357, Wakati Katibu wa Siasa na uenezi amechaguliwa Sitta Kija Mashalla  kwa kura 101.

Wajumbe wa kamati ya siasa waliochaguliwa ni Esta Simba 131 ,Issa Butwa kura 125  na Athanas Dotto kura 124 kwa upande UWT waliochaguliwa ni Grace Maumbuka kura 755 ,Esta  Simba kura 733 , Fatuma Kisabu kura 627 , Jilige Dotto kura 606 .na upande wa kundi la vijana waliochaguliwa ni  John Tugwa  kura 830, Jonathan Mnyela kura 747, Mayunga Ngokolo kura 602,na  Laurent Yohana kura 480.

Aidha kwa wajumbe wa halmashauri kuu  kupitia  jumuiya ya wazazi  waliochaguliwa ni Marco J  Bukwimba kura 310 na Issa \Butwa kura 207

Mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho wilaya Eng. Paul  Ndushi Jidayi  amewaagiza wanachama kuvunja makundiyaliyokuwepo kipindi cha uchaguzi huku akisisitiza kuwa kila mtu awajibike kwa nafasi yake na asiyeweza ajiondoe mapema.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata