18 WATIWA MBARONI KWA MAUAJI

Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya mkoani Mara, linawashikilia watu 18 kwa tuhuma za mauaji baada ya kumshambulia kisha kumchoma mishale yenye sumu mkazi mmoja wa kitongoji cha Mwara Bw. Magige Mesenda na kusababisha kifo chake.

Kamanda wa Polisi Kanda ya Tarime na Rorya, SACP Henry Mwaibambe, amesema kuwa kikundi hicho kimekuwa kikijihusisha na mauaji ya watu mbalimbali kimekamatwa kikiwa na silaha za jadi ambazo zimekuwa zikitumika kufanya vitendo hivyo vya mauaji.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata