WAZIRI ATANGAZA FURSA KWA WAWEKEZAJI

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles John Mwijage ameaomba wawekezaji wa viwanda nchini India waje hapa nchini kuwekeza kwenye sekta za viwanda.

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amedai kwamba kufika kwa wageni hao kutaleta chachu ya mabadiliko kwenye viwanda kwa kubadilishana uzoefu

Aidha Mh. Mwijage amewaomba wakulima wa kilimo cha mbaazi za aina mbalimbali walime kwa wingi ili kuendana na soko la nchini India ambapo nchini kwao zao hilo ni lulu.

Pia amewaomba wataalum wa Kompyuta kutoka nchini India kuja hapa nchini ili kubadilishana uzoefu na wataalam wa hapa nchini.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata